Jumapili, 24 Mei 2015

ASKOFU MCHUNGAJI MKUYU AKIHUBIRI NA KUFUNDISHA MANENO YA MUNGU KATIKA IBADA YA TATU.

Askofu Mchungaji Mkuyu akifundisha na kuhubiri maneno ya Mungu katika ibada ya tatu.


                               UJUMBE: KUJAZWA ROHO MTAKATIFU.


                           MAANDIKO: MATENDO YA MITUME 2:1-4

Nayo inasema:


1. Hata ilipotimia siku ya pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi,ukaijaza nyumba yote waliokuwa wameketi.

3. Kukawatokea ndimi zilizogawanyika,kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4. Wote wakajazwa Roho mtakatifu , wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.






        Watumishi wa Mungu wa kizazi hiki cha leo yatupasa tujazwe roho mtakatifu na kuweza kunena kwa lugha mpya, maana kuna faida kubwa sana kama mkristo akiwa anaweza kunena kwa lugha mpya, maana hata wakati unawasiliana na Mungu na kumshirikisha maombi yako, ikifika wakati umejazwa Roho mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha mpya hapo hata shetani mwenyewe hawezi kuisikia iyo lugha ya Roho mtakatifu, kwa hiyo kuna faida kubwa sana kujazwa Roho mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha mpya.

0 maoni:

Chapisha Maoni